August 6, 2018


Wakati pambano la Ngao ya Hisani likitarajiwa kushika kasi Agosti 19 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, tayari maandalizi ya kuuandaa Uwanja huo yameshaanza.

Taarifa kutoka Mwanza zinaeleza kuwa tayari ukarabati wa Uwanja umeanza kufanyiwa marekebisho ikiwemo vyoo vyake pamoja na ukataji nyasi ndani ya pichi.

Mbali na ukarabati huo, imeelezwa hali ya ulinzi na usalama kuzunguka eneo zima la Uwanja itakuwepo ili kuufanya kila kitu kiende vema kuelekea mechi hiyo kubwa.

Simba na Mtibwa zitakutana kucheza mechi hiyo itakayokuwa inakaribisha rasmi pazia la Ligi Kuu Bara Agosti 22 2018.

Mtibwa wanaenda kukipiga na Simba kutokana na kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho 'Azam Sports Federation Cup' kwa kuifunga Singida United jumla ya mabao 3-2 huku Simba ikitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic