August 6, 2018


Winga wa Yanga, Mrisho Khalfan Ngassa amefunguka na kuwataka wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kuwa watulivu kipindi hiki cha mpito.

Ngassa ambaye msimu uliopita alikuwa akiichezea Ndanda FC ya Mtwara, amesema kuelekea msimu ujao kikosi kitafanya mambo makubwa ambayo wengi hawatarajii.

Kauli hiyo imekuwa kutokana na mashabiki wengi wa timu kuvunjika moyo juu ya mwenendo wa Yanga ulivyo hivi sasa ambapo klabu imeyumba kiuchumi na kusababisha wengi kuwa na wasiwasi kuelekea msimu ujao.

Mchezaji huyo ameeleza kutokana na namna wanavyojifua hivi sasa mjini Morogoro ambapo wameweka kambi maalum kwa ajili ya kuwawinda USM Alger, imekuwa na maendeleo mazuri.

Kutokana na kambi hiyo, Ngassa anamini programu ambazo wanapewa na Kocha, Mkongomani, Mwinyi Zahera, zitawafanya wachezaji kuwa katika morali nzuri na kuonesha upinzani mzito ikiwemo Simba msimu ujao.

Yanga inajiandaa kucheza na Alger Agosti 19 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Saalam ukiwa ni mchezo wa mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ule wa kwanza kupoteza kwa mabao 4-0 huko Algiers, Algeria.

3 COMMENTS:

  1. Msikidhara kisu kibutu kwasababu kikikata kinaumiza kweli na nawahadharisha wale wenye kiburi. Sisimizi mwenye harakati ni bora kuliko simba mwenye kusinzia. Nyinyi dharauni tu kwani kutangulia sio kufika mwanzo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Washabiki wa Yanga mnapenda kudanganywa sana..sasa huyo fala atawaambia nini,keshachuja sasa hivi huyo ni mganga njaa...hivi kweli yanga hii ni ya kujifariji namna hiyo...angalieni msije mkaanza kumbebesha virago kocha...alafu hamna jipya kabla ya kurudiana na gor mahia mlitambaa kwenye viombo vya habari mnataka kupindua meza kibabe mara kocha oooh nimepata dawa ya gor mahia tupo tayari kurudisha kisasi matokeo yake mkachezea za kutosha tu...sasa hivi kila mkitaka kujifaraji mtataka kufanana na MNYAMA MBAYA SIMBA..ooh mara tutawashangaza simba kweli mkiwafunga Simba lazima tushangae kwa sababu uwezo wenu mdogo kama mlivvyotoa mfano wa sisimizi kweli nyie ni sisimizi na SISI NI SIMBA BHANAAAA

      Delete
  2. lugha uliyotumia ndugu yetu sio ya kiungwana huwezi muita binaadam mwenzio fala !! malezi ni muhimu sana !!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic