KAMATI YA ROHO MBAYA SIMBA KUKUTANA KWA AJILI YA KOTOKO NA MTIBWA
Wakati kikosi cha Simba kikitarajiwa kutua leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni baada ya kambi ya wiki mbili huko Uturuki kumalizika, Kamati ya Roho Mbaya kutoka Tawi la Wekundu wa Terminal imetangaza kukutana.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa kundi hilo, Masoud Chike, amesema kamati hiyo inakutana na wanachama wake wa tawi hilo kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kuwamaliza Asante Kotoko ambayo watacheza nayo Agosti 8 siku ya Simba Day.
Aidha, Chike amesema baada ya mchezo huo mipango ya kuhakikisha Mtibwa anakaa katika mchezo wa Ngao ya Hisani Agosti 19 utakaopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, itaendelea.
Chike amefunguka akisema lengo kubwa la kufanya hivyo ni kuhakikisha Simba inafanya vema zaidi kuelekea msimu ujao wa ligi ikiwa ni mipango ya kuhakikisha timu yao inatwaa ubingwa mara tatu mfululizo.
0 COMMENTS:
Post a Comment