August 15, 2018






Na Saleh Ally
KUMEKUWA na mjadala mkuu kuhusiana na taarifa kuwa Nahodha wa Yanga, Nadir Ali Haroub ‘Cannavaro’ alipewa kiroba cha kilo 20 na baadhi ya mashabiki wa Yanga.

Taarifa hizo zinaenezwa kila sehemu lakini uongozi ulieleza kwamba ulitoa ngao ya heshima kwake lakini wako mashabiki waliotoa kitunza maji kwa ajili yake ikiwa ni kama sehemu ya shukurani.

Wanaoanzisha mjadala wengi wamekuwa wakizungumzia suala la kudhihaki, wakisisitiza kwamba Yanga imekuwa na njaa ndiyo maana mambo ni magumu hata Cannavaro amepewa mchele kiasi cha kilo 20 tu.

Kwa kuwa uongozi umesisitiza kwamba alipewa ngao kama tuzo ya heshima, tunaweza kuliweka kando suala la kiroba na kama lingekuwepo, basi tutoe heshima kubwa kwa ambaye aliona awaache nyumbani kwake na kumjali Cannavaro kwa heshima kubwa ambayo anastahili. Hii ni sehemu ya upendo.

Ukiachana na yote, nimeamua kuandika kwa ajili ya kuwakumbusha wapenda soka nchini kuhusiana na Cannavaro, nahodha wa Yanga wa aina yake na mwanadamu ambaye hakukubalika kwa muda mwingi lakini akaendelea kucheza kwa kiwango cha juu kwa muda wote.

Hakuna aliyewahi kusema Cannavaro mlevi au mtovu wa nidhamu, wengi walilalama kuhusiana na uchezaji wake wa kibabe, wakisema anaumiza wenzake. Lakini hawakuwa na takwimu zinazowalinda wala Cannavaro hakuwa na rekodi mbaya ya kadi nyingi sana za njano au nyekundu.

Cannavaro aliendelea kuwa beki bora aliyekabana karibu na kila mshambulizi hatari uliyemjua. Leo anastaafu akifa na mafanikio makubwa kwa mataji huenda kuliko aslimia 99 ya wachezaji waliowahi kucheza Ligi Kuu Bara kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita.


Makombe ya ubingwa wa Ligi Kuu Bara anayo nane, ubingwa wa Kombe la Shirikisho, Kombe la Kagame mara mbili lakini katika kabati lake amehifadhi Ngao za Jamii nne.

Huyu si mtu wa mchezomchezo na hakika katika mpira wa hapa nyumbani anastahili kuwa mfano wa kuigwa na isiwe wa kuigwa kwa mashabiki na watu wa Yanga pekee.

Cannavaro alikuwa nahodha wa timu ya taifa, nahodha aliyefanya vizuri akijituma na kujitolea kwa juhudi kubwa hadi alipovurugwa na aliyekuwa kocha wake wakati huo, Charles Boniface Mkwasa.

Cannavaro hapaswi kuheshimiwa na Yanga na kudhihakiwa na Simba eti kwa kuwa ni watani. Cannavaro anastahili heshima ya kitaifa na TFF wanapaswa kukumbuka kumtuza kwa kuwa amekuwa ni nahodha bora, sahihi na mpiganaji kwa taifa lake.

Msiache Cannavaro akaondoka mkimdhihaki na maneno ya viroba huku mkijisahaulisha yake bora kwa zaidi ya miaka 15 katika mpira wa Tanzania akiwa bora kwa kiwango cha uwanjani, nidhamu na maisha nje ya mpira.

Cannavaro anatakiwa kuendelea kubaki katika vitabu vyetu kama mtu sahihi. Mtu atakayetumika kuwakumbusha wanaokua na kuwaamsha kwa kuwaaminisha wale ambao walikuwa wakiamini haiwezekani ili kutenda na kufanikisha kile kilichoonekana kisingewezekana.


Kama kutakuwa na shabiki au mwanachama wa Simba anataka kumdharau Cannavaro, basi ni aina ya watu waliongia katika mpira hivi karibuni au wale ambao wanaamini kuupenda mpira na kuufurahia ni kuwa na uwezo wa kuzomea pekee.

Angalia upinzani wa FC Barcelona na Real Madrid, ni zaidi ya upinzani na uadui. Unaanzia uwanjani, kimkoa, kijimbo, kisiasa na hata kifamilia. Lakini mara zote uliona Real Madrid wakisimama na kumpigia makofi ya hedhima Andres Iniesta tena katika mechi ya El Clasico.

Wanaofanya vile ni Wahispania, wanaonyesha kuikubali kazi ya Iniesta hasa katika kikosi chao cha timu ya taifa. Lakini wanataka kuthibitisha kuwa wanamthamini kama mfano bora katika taifa lao la Hispania.

Kweli Tanzania hatujafika mbali sana, lakini Cannavaro ana mambo ya kuthaminiwa na kupewa sifa katika taifa letu na si Yanga pekee. Tafadhali tusimdhihaki kwa kuwa hastahili hicho.

Nimekuwa nikitamani siku moja kuona Simba wakimpigia makofi Cannavaro kumpongeza ili kuonyesha nasi tunabadilika. Lakini Cannavaro naye awashukuru Simba kwa kazi nzuri ya kumfanya awe imara kwa kuwa changamoto zao zilimfanya yeye azidi kuwa bora hadi kufikia alipo.



8 COMMENTS:

  1. Nakumbuka matukio mawili ya kadi zake nyekundu.

    1- Shamba la bibi, Ruvu vs Yanga alilambwa nyekundu akiwa kinda kabisa alipozozana na mshambuliaji Wa Ruvu Chirwa.

    2- hii ni kati ya Yanga vs Azam hapa shukrani pekee ziende kwa NURDIN BAKAR naamini Cannavaro siku ile ndo ilikuwa ameamua iwe mwisho wake Wa kucheza soka.

    Mwamuzi Israel Nkongo aliamua uamuzi Wa maana kumpa kadi Canavaro akiwa mbaali kwani spidi aliyotoka nayo Canavaro kwenda kumvaa refa nilikuwa ya hatari.

    Shukuru Mungu akadakwa na Nurdin Bakar wakaanguka chini.

    Vinginevyo kipigo kile TFF ingemfungia maisha.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Upo sahihi alidhamiria kumuumiza. Hivi zile vurugu za kutoka kumpiga Refa kichapo cha Azam ? hakuna mmojawapo waliogeuka maboksa?
      Mimi namuheshimu kwa msimamo wake wa kujiuzulu time ya taifa pale mocha Mkwasa alipomteua Samata kwa Captain wakati Cannavaro hakujulishwa na ilikuwa kumdhalilisha. Pale nilimsifu kuwa anao msimamo.

      Delete
  2. Nakumbuka matukio mawili ya kadi zake nyekundu.

    1- Shamba la bibi, Ruvu vs Yanga alilambwa nyekundu akiwa kinda kabisa alipozozana na mshambuliaji Wa Ruvu Chirwa.

    2- hii ni kati ya Yanga vs Azam hapa shukrani pekee ziende kwa NURDIN BAKAR naamini Cannavaro siku ile ndo ilikuwa ameamua iwe mwisho wake Wa kucheza soka.

    Mwamuzi Israel Nkongo aliamua uamuzi Wa maana kumpa kadi Canavaro akiwa mbaali kwani spidi aliyotoka nayo Canavaro kwenda kumvaa refa nilikuwa ya hatari.

    Shukuru Mungu akadakwa na Nurdin Bakar wakaanguka chini.

    Vinginevyo kipigo kile TFF ingemfungia maisha.

    ReplyDelete
  3. Umesema ni suala la utani halafu eti unasema anadhihakiwa. We vipi? Suala la kumheshimu au kutoheshimu kazi yake ni suala personal na wala si la lazima. Wanayanga pekee ndio wanaopaswa kumheshimu na kuthamini mchango wake, wanasimba kawafanyia nini hadi waheshimu uwezo wake? Hana heshima yoyote katika timu ya taifa zaidi ya wachezaji wengine, sasa washabiki wa simba wamheshimu kwa lipi? Umezungumzia suala la Iniesta Kupigiwa makofi na washabiki wa Madridi, lakini umesahau kuwa hakuna hata siku moja mashabiki wa Cataluna walishawahi kusimama na kukubali uwezo wa mchezaji wowote wa Madrid. Sasa hujiulizi hilo. Mimi kama mimi namjua na kumsikia muda mwingi Nadir Haroub katika soka la bongo kwa mda mwingi lakini sina lolote la kumheshimu kwa uwezo wake. FULL STOP!

    ReplyDelete
  4. Unaona yanga walichofanya ni sawa kwa sifa alizonazo Nadir kuandaa mechi ya kumuaga na mawenzi market kweli...kwann angalau wasingesubiri mechi yao ya kwanza ya ligi uwanja wa wa taifa ndo iwe maalum kumuaga na kumpa tuzo walomuandalia

    ReplyDelete
  5. kitaifa hana sifa baada ya kugomea kujiunga na timu ya Taifa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic