August 5, 2018


Imeelezwa kuwa Kaimu Rais wa klabu ya Simba, Salim Abdallah 'Try Again' amefunguka juu ya hali ngumu kiuchumi wanayopitia watani zao wa jadi Yanga katika kipindi hiki.

Abdallah ambaye amekaimu nafasi hiyo kutokwa kwa Rais wa klabu Evans Aveva ambaye ameshikiliwa na jeshi la polisi kutokana na kesi ya ubadhirifu wa fedha, amesema hawafurahii kuona Yanga ipo katika hali ya mpito hivi sasa.

Kaimu huyo ameeleza namna mwenendo na hali ya Yanga ilivyo sasa ifikie kipindi uongozi wa timu hiyo ukae chini na kujipanga namna ya kuikomboa timu iweze kurejesha nguvu yake kama mwanzo.

Abdallah amefunguka kwa kueleza kuwa Yanga na Simba wote wanadhaminiwa na Kampuni ya Bahati Nasibu ya SportPesa ambayo inatoa fedha sawa kwa timu hizo mbili huku akishindwa kuelewa tatizo linatoka wapi.

Kutokana na mwenendo wa Yanga namna unavyoenda, Abdallah ameshauri ifikie hatua viongozi wa klabu hiyo wakae chini na kujadili juu ya kutatua matatizo ambayo yanaifanya klabu kuwa katika hali mbaya, kitu ambacho kwake na uongozi wa Simba kwa ujumla hawafurahishwi nacho.




1 COMMENTS:

  1. Mbona kuna mambo mengi ya kufanya lazima kila siku wakiamka waiongelee yanga acheni hizo huo n ushabikia usiofaa ,toeni basi fedha,mnapiga kelele fedha za muhindi hizo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic