August 6, 2018


Na George Mganga

Wakati zikiwa zimesalia siku kadhaa kuelekea kufunguliwa kwa pazia la michuano ya Ligi Kuu Bara, unaambiwa klabu ya Ndanda bado haijaanza maandalizi.

Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa timu hiyo kupitia Radio EFM, Malale Hamsini, amesema Ndanda inakabiliwa na suala la ukata wa fedha jambo ambalo limepelekea maandalizi kuchelewa kuanza.

Hamsini ameeleza tatizo la kukosekana kwa fedha limekuwa likiipa wakati mgumu Ndanda kuelekea msimu ujao ambapo utekelezaji wa majuku ikiwemo fedha za wachezaji imekuwa ni tatizo.

Mbali na ukata wa fedha, Hamsini amesema wachezaji wengi waliokuwa katika kikosi cha kwanza wamesajiliwa na klabu kadhaa za Ligi Kuu jambo ambalo linawapa wakati mgumu wa kujipanga mpya kuelekea ligi kuanza.

"Bado mpaka sasa hatujaanza maandalizi kutokana na hali ya ukata wa fedha, vilevile wachezaji wangu wengi wameshachukuliwa na baadhi ya klabu jambo ambalo linaleta wakati mguu wa sisi kujipanga upya" alisema.

Hivi karibuni, uongozi wa Kagera Sugar ulitangaza kuingia mikataba na wa wachezaji takribani 7 wa Ndanda baada ya mabosi wa timu hiyo kushindwa kufiia mwafaka wa kuongea na wachezaji ili waweze kusalia Ndanda kuongeza mikataba mingine.

1 COMMENTS:

  1. Mkianza kuzidiwa maarifa mnaanza ooooh! Marefa wanazibeba timu fulani!!!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic