Timu ya Ruvu Shooting imekubali kufungwa mabao 2-1 na Tandahimba City katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Makonga uliopo Makonga wilayani Newala mkoani Mtwara.
Katika mchezo huo uliokuwa maalum kwa ajili ya uzinduzi wa Tawi la Mashabiki wa Ruvu Shooting wa Makonga, mabao ya Tandahimba yote yamefungwa na Sadati Mpochi dakika ya 8 na 51, huku lile la Ruvu Shooting likifungwa na Fully Zulu Maganga dakika ya 32.
Katika mchezo huo, kandanda safi lilionyeshwa na pande zote jambo ambalo mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Newala, Bi Aziza Mwangosongo aliwapongeza wote.
Mashabiki wengi waliojitokeza katika mchezo huo, kabla ya kuanza kwa mchezo wenyewe walikuwa wakisikika wakisema wanahitaji kumuona Masau Bwire kwani ndiye waliyemfuata.
Baadae Masau akapata nafasi ya kuwasalimia mashabiki hao ambapo mashabiki hao walionyesha furaha yao.
Huo...uwanja si rafiki kwa afya za wacheaawa
ReplyDelete