August 16, 2018


Beki wa Manchester United ya Uingereza, Antonio Valencia ameonyesha hisia zake juu ya kitendo cha mchezaji wa timu ya taifa ya Burundi ya vijana chini ya umri wa miaka 17 (U17) kumchezea rafu mbaya nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17, ‘Serengeti Boys’, Morris Abraham kwenye mchezo wa kundi A, michuano ya kufuzu fainali za Afrika kwa Vijana U17.

Valencia ameposti kipande cha video kwenye ukurasa wake wa Instagram kikionyesha uwezo mkubwa wa kumiliki mpira uliyofanywa na Morris Abraham wakati akijaribu kuwatoka mabeki wa Burundi jambo lililosabaisha mchezaji huyo wa Burundi kumchezea rafu mbaya ya kiatu cha shingo na kuanguka kisha kumkanyaga kwenye paja.

Watanzania wengi wametoa maoni yao kwenye ukurasa wa Valencia baada ya kuweka video hiyo huku tukio hilo likiwa limesambaa kwa wapenzi wengi wa soka duniani. Valencia alisajiliwa kama winga mwaka 2009 na kujikuta akiwa bora zaidi kwenye safu ya ulinzi ambapo imempelekea kuwa miongoni mwa wachezaji muhimu.

Kwenye mchezo huo wa kwanza wa kundi A, vijana wa Tanzania waliibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2 – 1 dhidi ya Burundi mabao yakifungwa na Kelvin John dakika ya 11, Agiri Ngoda akifunga dakika ya 29 wakati la Burundi likifungwa na Munaba Edson dakika ya 20. Michuano hiyo ya kufuzu fainali za Africa kwa Vijana U17 yameanza siku ya Jumamosi Agosti 11 na kutarajiwa kufikia tamati yake Agosti 26,2018.


2 COMMENTS:

  1. MIMI NILITARAJIA REFA KUMPA KADI MCHEZAJI WA BURUNDI LAKINI AJABU HAKUFANYA HIVYO. NI RAFU MBAYA SANA YA MAKUSUDI. NILITAMANI MCHEZAJI MWENYEWE WA BURUNDI AJITOKEZE KUOMBA SAMAHANI KWA MCHEZAJI WA TANZANIA LAKINI WAPI HAJAONA KOSA LAKE KAKAA KIMYA. BASI CHAMA CHAKE CHA SOKA CHA BURUNDI KIOMBE RADHI KWA MCHEZO MBAYA. NACHO KIMEKAA KIMYA. NA YULE REFA NILITEGEMEA CECAFA WANGEMSIMAMISHA KUCHEZESHA NA KUCHUKULIWA HATUA ZA KINIDHAMU LAKINI WAPI CECAFA WAPO KIMYAAAA. TFF BASI JITOKEZENI KULAANI KITENDO ALICHOFANYIWA MCHEZAJI WENU PASIPO REFARII KUCHUKUA HATUA STAHIKI KWA ALIYECHEZA RAFU ILE, WAPI TFF NAYO KIMYAA. INA MAAANA USTAARABU HAKUNA MPIRANI?MCHEZAJI ALIYEFANYIWA RAFU MBAYA ATASEMEWA NA NANI? SISI MASHABIKI MAGAZETINI? LIPO TATIZO. INASUMBUA AKILINI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nimeguswa na jambo hili. Mtu mwenye namba za kuwasiliana na CECAFA, CAF, FIFA naziomba

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic