SIMBA NA YANGA ZATAMBA MIKOANI
Na George Mganga
Kikosi cha wekundu wa Msimbazi, Simba kimeiba na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Arusha United katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Arusha leo.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Simba wamejipatia mabao yao mawili kupitia kwa Emmanuel Okwi huku la Arusha United likiwekwa kimiani na Kabunda.
Simba wamecheza mechi hiyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Mtibwa Sugar Agosti 18 utakaopigwa Uwanja wa CCm Kirumba, Mwanza.
Wakati huo watani zao wa jadi Yanga, nao wameeendeleza wimbi la ushindi huko Morogoro kwa kuweza kuilaza Mkamba Rangers FC ya Daraja la Pili kwa bao 1-0.
Bao pekee la Yanga limewekwa kimiani na kiungo Mkongomani, Papy Tshishimbi mnamo dakika ya 85 ya kipindi cha pili.
0 COMMENTS:
Post a Comment