August 9, 2018


Na George Mganga

Wakati tamasha la Simba Day likifana jana kwa maelfu ya mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi ndani ya dimba la taifa, Dar es Salaam, kuna walakini wa wachezaji wawili kuendelea kuwepo msimu ujao.

Katika tamasha hilo ambalo kufanyika kila mwaka ifikiapo Agosti 8, wachezaji wawili wa timu hiyo, Mrwanda Haruna Niyonzima na Mganda Juuko Murushid hawakutajwa katika orodha ya wachezaji wa msimu ujao.

Wachezaji hao walikosekana katika orodha kutokana na kutokuwepo kwao huku kukizua maswali kama wanaweza wakawepo kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara unaotaraji kuanza Agosti 22.

Ikumbukwe Simba ilitoa likizo kwa wachezaji wake wa kikosi cha kwanza baada ya msimu uliopita kumalizika huku Niyonzima naye alipewa baada ya SportPesa Super Cup kumalizika lakini akashindwa kurejea kwa wakati mwafaka.

Kuchelewa kurejea kwa Niyonzima kumewaacha wanachama na mashabiki mpaka viongozi wa Simba huku kukiwa na hatihati ya uwepo wake ndani ya kikosi cha msimu ujao baada ya kukosekana Simba Day jana.

Hata hivyo Niyonzima bado amesalia na mkataba wa mwaka mmoja ndani ya mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara ambapo baada ya kujiunga nao alisaini miaka miwili.

Aidha, kuhusiana na Murushid awali uongozi ulieleza kuwa amekwenda Afrika Kusini kukamilisha mipango ya kujiunga na SuperSport United FC lakini baadaye kukaja tena taarifa kuwa ameshindwa kufikia mwafaka na klabu hiyo na ikaripotiwa amesharejea nchini.

Baada ya kuripotiwa kuwa Murushid amesharejea Dar es Salaam, jana katika tamasha la Simba Day naye hakutangazwa na kupelekea kuibua mjadala kama atakuwepo katika kikosi cha msimu ujao.

Katika tamasha hil kubwa, Simba ilicheza na Asante Kotoko kutoka Ghana na kwenda sare ya 1-1 huku bao la Simba likiwekwa kimiani na Emmanuel Okwi.

3 COMMENTS:

  1. Hongera Simba kwa uwezo mkubwa sana waloouonesha baada ya wiki mbili tu ys Kocha Mbegiji. Simba ingeweza kuondoka hata na mabao matatu wacha na penelti iliuopotea na walitawala na kupoteza fursa nyingi.

    ReplyDelete
  2. Kumbe kweli nyinyi ni wazito wa kupata na kutuletea habari. Kwa taarifa yako Juuko Murshidi keshasajiliwa na klabu yake ya Vipers ya Uganda tangu siku ya tarehe 2 mwezi wa 8. Siku 6 nzima hakuna chimba cha habari cha tanzania kinajua wakati habari hii iko kwemye gazeti zote za Uganda na pia kwenye website maarufu ya mchezo ya kawowo. Ni usajili uliotingisha kati ya wachezaji 9 waliosajiliwa na vipers msimu huu

    ReplyDelete
  3. Ni kweli Juuko kajiunga na Vipers ambayo ni timu yake ya zamani kwa dau la usajili lililotikisa Uganda

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic