YANGA YAJIBU MAPIGO SIMBA, YAITWANGA TANZANITE 5-1
Na George Mganga
Kikosi cha Yanga kimeanza kuonesha ubabe wa mechi zake za kirafiki huko Morogoro kwa kuikandamiza kipigo cha mbwa koko Tanzania Academy cha mabao 5-1.
Katika mchezo huo uliokuwa wa kwanza kwa, mabao ya Yanga yalifungwa na Deus Kaseke, Emmanuel Martin, Maka Edward, Heritier Makambo na Mrisho Ngassa.
Yanga imecheza mchezo huo na kituo hicho cha kukuza vijana ambao ulikuwa ni pendekezo la Kocha Mkongomani, Mwinyi Zahera, kwa ajili ya kuwapima wachezajiw ake vizuri.
Zahera alihitaji timu ya daraja la chini ili kuona wachezaji wake namna walivyopokea mafunzo yake kwa takribani siku tano ambazo wamefikisha Morogoro tangu waweke kambi mjini humo.
Yanga imekipiga na Tanzanite Academy ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Agosti 19.
Huu utani mwengine haufai Yanga ajibu mapigo kwa Simba kwa kumfunga nani?
ReplyDeleteHaha haha haha kwa kuwafunga kijana wanaojifunza soka katika kituo cha kuinua soka la vijana wa mjini morogoro (Tanzania Academy) wengi wao wana miaka kati 16 na 17 waliookotezwa katika vitongoji vya Moro
ReplyDeleteDuuh wakimataifa wanajipima na academy?
ReplyDeleteDuuh wakimataifa wanajipima na academy?
ReplyDeleteYanga yapeleka salamu kwa Simba kwakuishibisha magoli timu kali ya mchangani. Tutakumbuka kuwa Kocha Zahera alitamka kuwa watafanya sapraizi na kweli wameifanya na hiyo ni pia kwa wale walioukwa wakijiona nyota na walo waliotakia mabaya yanga kudhani bila yao yanga itashindwa. Wakae upande wawaache wanaume kaxi yao
ReplyDeleteUkiwa na wachezaji wapya na msimu mpya ndio inavyotakiwa unaanz na team dhaifu.
ReplyDeleteMfano Everton ameifunga timu ya mchangani goli 22 pia Arsenal alishinda goli 8-0 alikazarika Simba dhidi ya timu ya umoja wa madereva wa waendesha Tax wa Kiparestina nchini Uturuki
Huyu mwandishi boya kweli kweli
ReplyDeleteHivi nyie wanasimba mnapenda kushadadia mambo ya yanga hivi nyinyi mbona mlecheza na umoja wa madereva tax wa kipalestana uturuki alafu yanga wako kimya na wiki end hii mnaenda kucheza na timu kutoka ruandwa ligi sijui hiyo barcelona
ReplyDelete