KANGI LUGOLA ATANGAZA VITA KALI NA WAUZA JEZI FEKI SIMBA DAY
Na George Mganga
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye ni Mbunge wa jimbo la Mwibara, Bunda, Kangi Lugola, ametangaza vita na walanguzi wote wa jezi feki za Simba.
Hatua hiyo imekuja kufuatia kuwepo kwa baadhi wa wafanyabiashara wanaotengeneza jezi feki kisha kuziuza mtaani kwa njia za magendo na kujipatia faida kinyemela.
Lugola amesema kwa sasa ameanza vita rasmi na watu wote waoanfanua biashara hiyo ya utengenezaji wa jezi feki ambazo ameeleza zinainyima klabu mapato ambayo imekuya ikiyapata kutokana na jezi asili inazozalisha.
Waziri huyo ametamka hayo katika tamasha kubwa la Simba Day ambalo lilifanyika jana katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo Simba ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana na kwenda sare ya 1-1.
"Natangaza vita rasmi na wale wote wanauza jezi feki, wanaisababisha klabu kukosa mapato ambayo wanapaswa kuyapata kutokana na jezi orijino wanazotengeneza, nitashughulika nao.
0 COMMENTS:
Post a Comment