September 25, 2018


Na George Mganga

Baada ya baadhi ya taarifa kuibuka zikieleza kuwa kiungo fundi na mjanja wa klabu ya Yanga, Feisal Salum 'Fei Toto' kuwa atakosekana kwenye mechi ya watani wa jadi dhidi ya Simba, uongozi Yanga umethibitisha atakuwepo.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, ameeleza kuwa Toto atakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachocheza na Simba Septemba 30 2018.

Toto amekuwa pia mmoja wa wachezaji walioelekea mjini Morogoro jana kwa ajili ya kambi maalum kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba.

Yanga imeamua kuliacha jiji ili kuwapa utulivu wa aina yake wachezaji wake pia kuwaweka fiti kisaikolojia kwa ajili ya ajili ya kuhakikisha wanapigania alama tatu dhidi ya Simba.

Kikosi hicho kitarejea Dar es Salaam majira ya jioni Septemba 29 tayari kwa ajili ya kucheza na Simba Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic