September 25, 2018


Hitmaker wa Ngoma ya Salama, Mwanaisha Said ‘Dayna Nyange’ amesema kuwa, anajuta kusafiri Ulaya kwani kumemfanya kurudi upya kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva.

Akizungumza na Star Showbiz, Dayna alisema, alipata nafasi ya kutembelea baadhi ya nchi ikiwemo Marekani na nchi nyingine za Afrika kidogo na kukaa huko kwa zaidi ya miezi miwili bila kujihusisha na muziki wake jambo lililomfanya kupata wakati mgumu kuanza tena gemu.

“Nimejifunza mengi na najuta kutumia muda mrefu Ulaya, nimeachia Wimbo wa Salama lakini mapokezi yake si makubwa sana kama ilivyo nyimbo zangu nyingine na hii ni kwa sababu mashabiki walianza kunisahau,” alisema Dayna.

2 COMMENTS:

  1. wasanii wa kibongo bwana, yani kukaa nje miezi miwili tu drama zimeshaanza....au alitaka ijulikane km alikuwa nje ya nchi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic