September 24, 2018


Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, ameweka wazi kuwa, hana hofu yoyote kama itatokea anataka kutimuliwa kwa kuwa timu nyingi za Afrika, ikiwemo Simba, zimekosa malengo ya muda mrefu kwenye mchezo wa soka.

Kocha huyo aliyechukua mikoba ya Mfaransa, Pierre Lechantre, tayari amekuwa kwenye wakati mgumu kutokana na kuelezwa kutokuwa na maelewano mazuri na msaidizi wake, Mrundi, Masoud Djuma ambaye amemucha Dar katika mechi za mikoani wanazoendelea kucheza, huku pia matokeo yakionekana kutokuwa mazuri Msimbazi.

Kwa mujibuwa  Championi Jumatatu, Aussems amesema kuwa hawezi kuwa na hofu ya kutimuliwa kwenye timu hiyo kwa kuwa suala hilo ni kawaida kwa makocha.

“Niwe na hofu au niogope kufukuzwa kwa jambo gani labda ambalo linashangaza? Unajua kazi yangu ni kufundisha na walimu suala la kutimuliwa siyo geni, popote linatokea kwa wakati wowote, sasa nini kwangu cha kunifanya niogope?

“Kiukweli siwezi kuwa na hofu juu ya hilo, naijua vizuri kazi yangu ni ipi kama mwalimu, lakini tatizo limekuwa kubwa kwa sababu klabu nyingi za Afrika zimekosa malengo ya muda mrefu, ndiyo maana unaweza kuona ndani ya kipindi kifupi.

"timu inakuwa na makocha kibao ila imeshindwa kupata matokeo, hivyo ni jambo jema kuangalia malengo kama hayo anayotaka kufanya Mo (Mohamed Dewji),” alisema Aussems.

CHANZO: CHAMPIONI

2 COMMENTS:

  1. Bora umewapa makavu kweupe.Afukuzwe kwa lipi?Tubadilike

    ReplyDelete
  2. Hafukuzwi kocha Mzuri tu ila watanzania ni mambumbu. Licha yakuwa kocha lakini pia anamichongo kibao ya wachezaji wenye malengo yakwenda kucheza soka ulaya. Yaani ni moja kati ya makocha wachache wenye kujali maendeleo na maslahi ya mchezaji. Yaani TTF ndo washamleta Amunike ni jambo nzuri lakini makocha kama hawa wa Simba ndio wakuwa makocha wa timu ya Taifa kwani angelipigana kuhakikisha anakuwa na maprofessional wengi kwenye timu yake na uwezo wa kufanya hivyo anao. Sio siri Masoud Djuma anapigania kuwa kocha mkuu wa Simba na sio kama uwezo hana lakini kimaelengo ya muda mrefu kujenga timu yenye heshima basi kocha mtaalam wa kiwango cha Aussems kaja katika wakati sahihi kabisa. Unakumbuka kichuya aliwahi kumgomea Masoud Djuma kule Zanzibar usitarajie kuona vitu kama hivi vikitokea kwa huyu mzungu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic