BAADA YA KUREJEA NCHINI AKITOKEA MAMELODI, SINGIDA WATOA RIPOTI YA MCHEZAJI WAO
Na George Mganga
Mshambuliaji wa Singida United, Habib Kyombo aliyekuwa amesafiri kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya majirbio na klabu ya Mamelodi Sundowns amerejea nchini.
Kyombo tayari yuko na timu huko Singida baada ya kukamilisha majaribio na timu hiyo kongwe inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Singida United, Festo Sanga, amesema Mamelodi wamefurahishwa na kiwango cha mchezaji huyo kwa muda wote aliokuwa akijifua.
Mbali na kufuruhishwa, Sanga amesema klabu hiyo itafanya mazungumzo nao kuona namna ipi wanaweza wakamsajili ili aweze kutoa huduma yake kwao kwa siku za usoni.
Endapo dili za Kyombo kufanikiwa huko Afrika Kusini litatia tiki, atakuwa anaungana na Yahya Zayd pamoja na Abdi Banda ambao wanacheza soka lao nchini humo.







Usituzuge hana Level ya kuchezea Mamelodi Soundowm bana!
ReplyDeletekwani yahya zaid anachezea huko?
ReplyDeleteDUH YAHYA ZAYD YUKO AZAM
ReplyDelete