September 24, 2018


Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemwagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Eng. Kamwelwe kutangaza zabuni haraka kwa ajili ya kujenga kivuko kipya cha Ukara baada ya MV Nyerere kuzama. 

Ameagiza kivuko hicho kiwe na uwezo wa kubeba tani 50 na watu zaidi ya 200.

Kivuko hicho kipya kitakuwa na ukubwa mara mbili ya MV Nyerere kilichokuwa na tani 25 pekee na uwezo wa kubeba watu 101.

1 COMMENTS:

  1. Sina uhakika au ufahamu wa wajibu na majukumu ya watu wa usalama wa Taifa. Lakini kwa dhana ya haraka haraka mtu yeyote yule anajua neno usalama wa Taifa linajieleza wenyewe kuwa ni kukosi kazi cha kusimamia usalama wa Taifa lakini kiukweli hakuna Taifa litakaloitwa Taifa bila yakuwa na watu kwa hivyo usalama wa Taifa ni usalama watu sasa ajali kama ya Mv Nyerere watu wetu wa usalama wa walikuwa wapi? Neno usalama wa Taifa kimantiki ni jepesi kutamka lakini kiuhalisia wahudumu wanaohusika na majukumu hayo ya kulilinda taifa lolote lile duniani huwa sio watu wa kawaida na hii ni kutokana na unyeti wa kazi yao.Na kutokana na unyeti wa kzai yao na ndio hapo linapokuja neno(intelligence).Mtu wa kawaida akiitwa intelligence anakuwa mahiri kwa kiasi chake. Lakini askari anapoitwa intelligence mara nyingi huwa sio binaanadamu wa kawaida kiakili,kinguvu, kimaamuzi nakadhalika.Na kwa nchi yeyote ile nadhani sehemu kama Bandarini,Airport kwa maana ya uwanja wa undege, Mipakani yaani mipaka kati ya nchi na nchi ni sehemu ambazo watu wa usalama wa Taifa uwepo wao ni sawa na kumkuta Nyuki kwenye Sega au Mzinga wake.Na kwa maana ya askari wa usalama wa Taifa ni sawa na mtu mwenye jicho la mwewe yaani ule uwezo wa kuona vitu au mambo yatakayopelekea kuleta maafa kwa Taifa na kuyaripoti ili kudhibitiwa kabla hayajaleta madhara. Sasa inakuwaje tena serikali ihangaike kuunda kamati ya uchunguzi wa ajali badala ya kuwaachia polisi kuchungza? Ambao kwa kutumia taarifa za wenzao wa watu wa usalama wa Taifa ilitakiwa lazima wawe na mkanda mzima wa tukio kama itakuwa wanafanya kazi zao kisawasawa? Kazi ni kubwa kwa muheshimiwa raisi Magufuli to be honest. Badala ya kufokasi na ujenzi wa nchi hasa katika masuala ya uchumi lakini inambidi atoke huko na kuanza kufokasi na madhaifu ya watendaji wake kwanza. Ingekuwa vizuri wahusika wanaoguswa na uzembe hadi kutokea ajali hii kujiwajibisha wenyewe kabla ya kuwajibishwa. Lakini vile vile tuwe wawazi kabisa yakwamba kama taifa basi tujuwe yakwamba kuna mapungufu makubwa ndani vyombo vyetu vya usalama wa Taifa serikali lazima ifanye jitihada za kuwaongezea ufanisi labda mafunzo au kupanua wigo wao wa maeneo ya kazi kwani sidhani kama watu wa usalama wa taifa wapo kwa ajili ya masuala ya siasa tu. Kwani kwa wenzetu kila kitu kimeandaliwa taarifa zake za kiusalama 24/27 iwe uchumi au hata wanyama maporini wanaotoka pori moja kwenda jengine basi wahusika wanakuwa na taarifa zao itakuwaje sisi watu wanasafiri kiholela tu hata idadi yao haijulikani wangapi walikuweno kwenye meli au chombo kilikuwa na uzito gani?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic