Bocco atakosekana katika mchezo huo baada ya kupewa kadi nyekundu jana kwenye Uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga kwa kumpinga ngumi mchezaji wa Mwadui.
Nahodha huyo alipewa kadi nyekundu ya moja kwa moja ambaye itamfanya autazame mchezo huo akiwa jukwaani kwa sababu hatoweza kuwa sehemu ya kikosi kwa mujibu wa kanuni.
Simba inatamenyana na Yanga kwa mara ya kwanza msimu huu katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam huku ikiwa na kumbukumbu ya ushindi mara ya mwisho timu hizo zilipokutana.
Katika mchezo wa mwisho Simba ilifanikiwa kuifunga Yanga bao 1-0 kupitia SET PIECEES ya mpira wa faulo ulipigwa na Shiza Kichuya kisha kutiwa kimiani kwa kichwa na Erasto Nyoni.
Huwezi kujua kwa Simba ya sasa pengine kukosekana kwa Boko katika mechi ya watani sio habari njema kwa Yanga kwani ushindani wa namba ndani ya Simba kunamfanya kila mchzaji anaepata nafasi ya kucheza hasa wale waakiba kuwa makini zaidi. Hasa ukichukulia Kukosekana kwa boko inamaana Kagere sasa atasimama katikati katika mashambulizi hapo ndipo ninapoyaona mabao ya kitenge yakifungwa na Simba katika dakika ya 15 za kipindi cha kwanza wa mchezo.
ReplyDeleteWachezaji wajifunze kuwa wavumilivu pale wanapofanyiwa rafu na wengine pia nimpe hongera Boko kuwa mchezaji wa kwanza kuwa mchezaji mwenye magoli mengi toka ligi kuu kuanza ila kile alichokifanya ananikumbusha mchezaji Zidane du!
ReplyDelete