September 24, 2018


Baada ya taarifa awali kutoka zikieleza kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limempa siku tatu, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, Revocatus Kuuli kutoa ufafanuzi juu ya kusimamisha mchakato wa uchaguzi Simba, Mwenyekiti huyo ameibukua kivingine.

Kuuli ameeleza kuwa mpaka sasa bado hajapata barua hiyo ambayo ilielezwa kutoa maelezo juu ya kueleza kuwa alipata wapi mamlaka ya kufanya maamuzi hayo.

Mwenytkiti huyo amesema kuwa hakuna barua yoyote ambayo imetumwa kwake zaidi ya kusambazwa kwa taarifa mitandaoni peekee kitu ambacho ameeleza hakina ukweli.

Aidha, Kuuli amesema tayari Simba walishawasilisha mabadiliko yao kuhusiana na vipengele kadhaa ya mchakato wao ambavyo vilikuwa na uwalakaini.

Baada ya kuwasilisha, amezidi kuwasisitiza Simba kufuata kanuni na taratibu za uchaguzi ambapo mpaka sasa zoezi la kuwasilisha mapingamizi linaendelea.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic