September 12, 2018


Usiku wa kuamkia Septemba 9, 2018 ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, Posta jijini Dar historia katika mashindano ya ulimbwende iliandikwa baada ya mrembo kutoka Kinondoni, Queen Elizabeth Makune kuvishwa taji la Miss Tanzania 2018 huku skendo za mashindano hayo zikiandika historia.  

Tangu kuanza kwa mchakato wa mashindano hayo kwa mwaka huu, gazeti hili lilikuwa mzigoni kupekenyua skendo za washiriki lakini kwa mara ya kwanza waandishi wetu waliambulia patupu.

Kati ya skendo ambazo zimekuwa zikitikisa kwenye mashindano hayo katika miaka ya nyuma ni pamoja na baadhi ya washiriki kudanganya umri, kufoji vyeti, kuzaa na kuficha watoto pamoja na skendo za ngono lakini kwa mwaka huu mpaka mashindano hayo yanafikia hatua ya fainali, hakuna mrembo aliyeanikwa kwa skendo, jambo ambalo limewashangaza wengi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wadau wa mashindano hayo walisema kuwa, kwa ishu ya skendo mwaka huu mambo yamekuwa ni tofauti na miaka mingine hivyo historia imeandikwa.

“Unajua kila yanapofanyika mashindano haya, kuanzia ngazi za chini utasikia mshiriki flani anatembea na pedeshee flani, au utasikia mshiriki flani amedanganya umri lakini mwaka huu sijasikia.

 “Inawezekana ni kwa sababu waandaaji wamekuwa makini kuanzia huko chini lakini pia huenda skendo zimefichwa ila zitaibuliwa tu, ngoja tuone,” alisema Sakina Jamal wa Magomeni jijini Dar.

Naye Suma Kajio wa Sinza jijini Dar ambaye ni mdau ‘kindakindaki’ wa mashindano hayo alisema kuwa, hata baada ya kutangazwa kwa Queen kuwa mshindi alitarajia watu kuanza kuanika skendo zake lakini mpaka gazeti hili linakwenda kiwandani, mrembo huyo hakuwa na doa. Aidha, warembo 20 waliotinga fainali za mashindano hayo walipotembelea ofisi za magazeti ya Global siku chache kabla ya fainali walionekana kutotaka kuchafuka kwa namna yoyote huku kila mmoja akidai ni msafi.

SKENDO NI YA GARI TU

Mpaka mashindano hayo yanamalizika, skendo ambayo ilionekana kuyatafuna ni zawadi ya gari aina ya Daihatsu Terios Kid iliyotolewa kwani ilionekana kutokuwa na hadhi.

MSHINDI AONGEA NA RISASI

Mwandishi wetu alifanya jitihada za kuongea na Queen Elizabeth ‘22’ (mshindi) ambapo kwenye suala la skendo alipotezea maswali yote aliyoulizwa ila akafungukia baadhi ya maswali. Fuatilia mahojiano hayo mafupi hapa chini…

SWALI: Wewe ni mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA),

sasa umekuwa Miss Tanzania na utakuwa na mambo mengi, je una mpango wowote wa kusimama kwanza masomo?

Elizabeth: Chuo nitaendelea kama kawaida.

SWALI: Familia yako inakusapoti kwenye fani hii ukiwa bado upo masomoni?

Elizabeth: Wananisapoti sana, wako bega kwa bega na mimi na wamekuwa wakinitia moyo kuanzia ngazi ya awali kabisa.

SWALI: Inaonekana tasnia ya urembo unaipenda kutoka moyoni, ukilikosa taji la Miss World utajisikiaje?

Elizabeth: Nitaendelea kuitumikia jamii kama Miss Tanzania, nitaumia ila nitaona sawa tu.

SWALI: Unazungumziaje zawadi ya gari ulilopewa maana wadau wanasema siyo hadhi yako.

Elizabeth: (Kimya).

SWALI: Kuna wanaosema huenda ukalewa sifa baada ya kutwaa taji hilo, wewe unawaambia nini?

Elizabeth: (Kimya).

Kutoka Global Publishers

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic