September 19, 2018


Na George Mganga

Timu ya Yanga imeendelea kujiwekea malengo mazuri ya kupigania ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union.

Mchezo huo ulioshuhudiwa ukipigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ulizitikisa nyavu za wagosi wa kaya mnamo dakika ya 12 kupitia kwa Heritier Makambo 'Makambovic'.

Bai hilo limeisaidia Yanga kujikusanyia jumla ya alama 9 mpaka sasa ikishinda mechi zake zote tatu.

Katika mchezo huo, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera alimuanzisha kama kawaida kipa mkongomani Klaus Kindoki ambaye alipokea lawama kali katika mechi iliyopita.

Kindoki aliruhusu kufungwa mabao matatu matatu dhidi ya Stand United huku wakiibuka na ushindi wa mabao 4-3 lakini leo ameonekana kulitendea haki lango la timu yake.

3 COMMENTS:

  1. Wametamgulia kwa BAISKELI ya BARAFU! Tutawakuta Mlimani wakiyeyuka!

    ReplyDelete
  2. Kwa mpira waliocheza hata baiskeli ya barafu afadhali labda ya ice cream.

    ReplyDelete
  3. Kama ndiyo mpira huo na kuwasifia akina Makambo na Ngasa, hatuna timu mwaka huu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic