September 20, 2018


Inafahamia kuwa kucheza na Mbao kwa timu za Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Kirumba si mchezo lakini kocha wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems hana hofu ila anakwenda kwa tahadhari kubwa.

Msimu uliopita Simba ikiwa katika Uwanja wa CCM Kirumba ilifanikiwa kutoa sare na Mbao FC ya mabao 2-2 huku wafungaji wa mchezo huo wakiwa Shiza Kichuya na James Kotei.

Mzungu huyo wa Simba alisema kuwa maandalizi yake yapo vizuri na atapambana kuhakikisha anapata matokeo kwenye uwanja huo ambao aliutumia kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii na kuibuka na ushindi dhidi ya Mtibwa.

“Ni mechi ngumu ambayo tunahitaji kupambana kuweza kupata ushindi kwa upande wa uwanja ni changamoto lakini tumewahi kuutumia uwanja huu kwenye mechi ya Ngao ya Jamii hivyo tunaujua.

“Wachezaji wapo fiti kupambana na lengo ni kupata pointi tatu muhimu na kusonga mbele na tunaenda kwa tahadhari kubwa sababu tunawaheshimu wapinzani wetu hivyo tunaenda kupambana,” alisema Mbelgiji huyo.

Katika msafara wa Simba wachezaji ambao wamekosekana kwenye mchezo huo ni pamoja na Asante Kwasi, Mzamiru Yassin na Hassan Dilunga ambao ni wagonjwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic