September 19, 2018


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe,  amesema kamwe hatoachia kiti hicho kwa kusikiliza maneno ya watu wa nje ya chama ambao hata hawakumchagua.

Mbowe amesema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam wakati akitoa tathmini ya Chadema kuhusu uchaguzi mdogo wa wabunge na udiwani uliyofanyika Jumapikli iliyopita na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuibuka washindi.

“Uenyekiti wa CHADEMA ni kazi ngumu na ni msalaba, ni kazi isiyo na faida. Walionipa mamlaka ni wanachama wangu wa Chadema, wakinitaka niondoke hata kesho nitaaondoka tena na nitashangilia kabisa na sherehe, lakini siwezi kuondoka kwa kuambiwa na watu waliopo CCM kwamba Mbowe ondoka, siondoki!” amesema Freeman Mbowe.

4 COMMENTS:

  1. Hivi hii nayo ni moja ya habariza michezo na burudani? Au mimi ndyo nimeshindwa kuielewa hii blog?

    ReplyDelete
  2. Hahahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaa ama kweli!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Mbowe ni mwenyekiti wa maisha wa Chadema na kwa kauli yake hii anathibitisha ukweli huo ni diktat huyo.

    ReplyDelete
  4. Mbowe wewe endelea kushika kijiti tu ata mzee Mugabe nae aling'ang'ania kama wewe mwisho wakamtoa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic