September 12, 2018


Na George Mganga

Mshambuliaji Mtanzania anayekipiga katika klabu ya KRC Genk, Ubelgiji, amesema moja ya ndoto alizonazo ni kumiliki ndege binafsi.

Samatta ambaye siku kadhaa zilizopita alikuwa na Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu fainali za AFCON 2019, ameeleza kuwa ndoto hizo zimeanza japo akiamini si kila ndoto itaweza kutimia.

Mshambuliaji huyo ambaye ni tegemo hivi sasa kwenye kikosi cha KRG Genk, ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kutua nchini humo akitokea Tanzania kwa majukumu ya Taifa Stars.

"Ndoto za kumiliki ndege binafsi zimeanza baada ya kupiga picha hii, si kila ndoto inaweza kutimia ila acha vita ianze" ameandika hivyo.


Endapo ndoto za Samatta zitatimia, mchezaji huyo atakuwa anafuata nyayo za wachezaji wakubwa duniani waliotimiza malengo hayo ikiwemo Mreno, Cristiano Ronaldo anayekipiga Juventus ya Italia na wengineo.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic