September 12, 2018


Baada ya kufungiwa kwa mwaka mmoja pamoja na kupigwa faini ya shilingi milioni 4 za kitanzania kwa Meneja wa timu ya Simba, Richard Robert, Wanachama wa klabu hiyo wamesema wataanzisha mkakati wa kuhakikisha haki inatendeka.

Wanachama hao wamesema kwa sasa mipango yao ni kuhakikisha wanapaza sauti kuanzia kwenye vyombo vya habari ili kuweka mambo sawa mpaka kieleweke juu ya adhabu aliyofungiwa Meneja wao.

Kupitia Radio EFM, Mwanachama aliyewawakilisha wenzake anayejulikana kwa jina la Jose Munyama, amefunguka na kueleza wanaanzisha kampeni ya kimyakimya ili kulishinikiza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) watengue maamuzi hayo.

Munyama amesema TFF haijatenda haki kwani adhabu hiyo ni uonevu mtupu kwa Robert ambaye wanaamini hakuwa na makosa ya kupewa adhabu kubwa kiasi hicho.

Mwanachama huyo ameongeza kwa kuwataka TFF wakae upya kupitia kanuni na taratibu walizotumia kumfungia Robert kisha waje na majibu mapya ambayo yatakuwa yanaridhisha.

6 COMMENTS:

  1. Kwa uonevu huu ni kususia kwenda uwanjani kuisapoti Stars. Adhabu ya dhuluma kabisa.

    ReplyDelete
  2. Kwa upande mwengine naona baadhi ya viongozi wa TFF wamekuwa wakijenga tabia ya kutumia lugha isiyostahiki kama vile maneno kuhujumu timu ya taifa na ile kuhusu Mtibwa kudai pesa zao pale walipotamka eti sio Mtibwa waliotamka madai hayo kwani Mtibwa ilikuwa imestaarabika. Lugha kama hizi zitajenga chuki. Michezo hujenga mapenzi baina nchi na nchi na duniani kote kama ilivo kombe la dunia. Mpira sio siasa mpira ni kujenga urafiki na upendo. Jambo hili lishughulikiwe kabla ya kuharibika mambo na malalamiko yameshakuwa mengi na sio kams TFF za zamani zilizokuwa na kila aina ya busara tunsshuhudia sasa maneno ya kukatakata maamuzi ya ajabu na ya kibabe

    ReplyDelete
  3. Adhabu aliyopewa ni uonevu wa kupitiliza.TFF jiangalieni maana mnakoenda mtaparaganyika.kama mtakalia mambo ya vikao ya kufungia watu badala ya kutafuta wadhamini wa kuendesha ligi kuu basi mtaparaganyika tu.

    ReplyDelete
  4. Tff hawajawahi kupambana na nguvu ya umma dawa ni kuanzisha ampeni ya kususia mechi zao zote zinazochezeshwa hicho kiburi kitawaisha na tena wadhamini watawakimbia watanyooka kabisa tatizo jingine ni viongozi wa simba mabadiliko ya katiba waliyofanya wamejiweka wao wako chini ya TFF wakati katiba ya mwanzo haikuwa hivyo

    ReplyDelete
  5. TFF ijithamini kwasababu malalamiko yanazidi na isijifanye ina uwezo wa kufanya walitakalo kila kukicha wanaleta mapya na lugha za kibabe mapyam

    ReplyDelete
  6. TFF sio sifa kuanza kuvuruga hali nzuri ya mpira nchini inavyoendelea. Jambo dogo linaweza kuzaa kubwa. Nyinyi wenyewe mmevuruga suala la wachezaji wa Simba. Mnataka kusujudiwa sana. Acheni hizo hazijengi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic