October 27, 2018




KIUNGO mshambuliaji wa timu Yanga, Ibrahim Ajibu ambaye amekuwa msaada mkubwa ndani ya timu yupo fiti kuwavaa Lipuli katika mchezo wao unaofuata utakaochezwa Uwanja wa Taifa October 30.

 Mratibu wa Yanga, Hafidhi Saleh alisema kuwa hali za wachezaji wote zimeanza kuimarika hivyo leo wanatarajiwa kuanza mazoezi katika uwanja wa chuo cha polisi kujiandaa dhidi ya mchezo wao na Lipuli.

"Ajibu  pamoja na Papy Tshishimbi walikuwa nje kutokana na kusumbuliwa na majeruhi, mpaka sasa wote wanaendelea vizuri na tayari wanatarajiwa kuanza mazoezi yanayoanza leo kwa ajili ya mchezo unaofuata Ligi Kuu Bara .

Ajibu amehusika kwenye mabao 11 kati ya 15 ambayo wameshinda Yanga, aliukosa mchezo wa KMC kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya mgongo aliyoyapata katika mchezo waliocheza dhidi ya Alliance FC ambao Yanga walishinda kwa bao 1-0.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic