Dirisha dogo la usajili linafunguliwa Novemba 15 mwaka huu, tayari mambo ni moto kwani ndani ya Simba mshambuliaji Mohamed Rashid huenda akaonyeshwa mlango wa kutokea.
Rashidi ambaye alisajiliwa msimu huu akitokea Prisons kwa dau la Sh. Mil 30 na mshahara wake unaonyesha analipwa Mil. 3 ukijumlisha kwa miaka miwili aliyosaini jumla ataingiza Sh.102 Mil.
Habari kutoka ndani ya Simba zimesema kuwa kuna uwezekano mkubwa klabu hiyo kutoongeza mchezaji yoyote kwenye dirisha dogo zaidi ya kuangalia wale ambao hawapati nafassi sana wakawatoa kwa mkopo.
"Mpaka sasa Kocha anasema kikosi kimekamilika, kuna baadhi hawana sifa kuitumikia timu inabidi watafutiwe sehemu wakakuze uwezo, kati ya wachezaji hao ni Mohamed Rashidi, ni ngumu kupata nafasi mbele ya Emmanuel Okwi, John Bocco, Meddie Kagere, Shiza Kichuya, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Claytous Chama ambao wanacheza nafasi ambazo akicheza," ilielezwa.
Simba imejaza washambuliaji wengi kwenye kikosi chao kiasi kwamba wengine wamekuwa wakikosa nafasi ya kucheza, mpaka sasa Rashid amekuwa akitajwa kuwa mmoja kati ya wachezaji watakaoondolewa na kurudishwa Prisons kwani Patrick Aussems hajavutiwa na uwezo wake.
0 COMMENTS:
Post a Comment