October 13, 2018


DAR ES SALAAM: Msichana ambaye kwenye Mtandao wa Instagram anatumia jina la Martha.aint-na kudai ni mtoto wa Zarinah Hassan ‘Zari’ amekuwa gumzo kufuatia kitendo cha yeye kuposti picha zake nyingi akifanana ‘kopi raiti’ na Zari, Risasi Jumamosi limemsaka na kumbana.  Kutafutwa kwa mrembo huyo ambaye mi Zari mtupu kulikuja kifuatia wengi kutaka kumjua ni nani, yuko wapi na ilikuwaje akapotezana na Zari aliyedai ni mama yake.

NI KUPITIA DM

Kwenye mtandao wa Instagram kuna kitu kinaitwa Direct Messenger ‘DM’ ambapo mwandishi wetu aliingia huko na kumtumia meseji akijatambulisha kuwa anaandikia Gazeti la Risasi Jumamosi na ndipo mrembo huyo aliyedai yuko nchini Kenya alijibu; ‘naomba kitambulisho ili nijue kama wewe ni mwandishi kweli’.

Haikuwa tatizo, mwandishi alimtumia kitambulisho chake na hapo ndipo alipofunguka kuwa, yeye na Zari hawajakutana akiwa mkubwa ila ni mama yake kwa mujibu wa ndugu zake.

“Mimi na Zari hatujakutana, kwa sasa nipo nchini Kenya ila nikipata nafasi ya kuja Tanzania nitafanya mahojiano na media kwa kirefu,” alisema. Aidha, Martha alipohojiwa mambo mengi zaidi kuhusiana na Zari alihama DM lakini alimuahidi mwandishi kuwa atamtumia namba ya simu ili waongee kwa njia ya WhatsApp.

AKAUNTI YAKE ETI NI FEKI.

Hata hivyo, baadaye watu wa karibu na Zari walidai kuwa, akaunti hiyo ni feki kwani mmiliki halisi anaitwa Martha, mrembo aliyefanana na Zari lakini hajawahi kuposti mambo hayo ya kwamba ni mtoto wa Zari.

“Huyo ametengeneza akaunti feki, mbona mwenye akaunti yupo na ameshatoa angalizo kuwa akaunti nyingi zinatumia picha na majina yake, lakini si za kweli, yeye amefanana na Zari tu wapo wanaomfa-nanisha,” alisema mtu huyo wa karibu ambaye ni timu Zari.

SABABU YA KUFANA-NISHWA NA ZARI

Msichana huyo anafananishwa na Zari kwa sura, mavazi na vitu vingi. “Unajua ukiona mapozi ya mwanadada huyo ni lazima umfananishe na Zari, wamefanana kwa vitu mbalimbali,” alisema Jamila shabiki wao mtandaoni.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic