October 13, 2018


Nahodha wa kihistoria wa Klabu ya Yanga Nadir Haroub Ally Upapa, ‘Canavaro’ leo amegwa kwa mara ya pili tangu atangaze kustaafu kucheza soka, ambapo safari hii ilikuwa ni zamu ya wadau wa soka visiwani Zanzibar, mahali alikoanzia soka.  

Tukio hili limefanyika kabla ya kupigwa kwa mchezo wa kirafiki kati ya Malindi FC na Yanga, kwenye Uwanja wa Amaan visiwani humo mechi iliyomalizika kwa Yanga kupata ushindi wa mabao 2-0. 

Mchezo huo umepigwa kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar na kushuhudia Yanga ikipata bao lake la kwanza kupitia kwa Emmanuel Martin dakika ya 43 akiitumia vyema pasi ya Mrisho Ngasa. 

Bao la pili la Yanga limefungwa dakika ya 60 na Mrisho Ngasa mwenyewe akimalizia pasi ya Pius Buswita. 
Katika mchezo huo, Canavaro ambaye kwa sasa ni meneja wa Yanga hakuonekana dimbani kusakata kabumbu, ambapo mara baada ya mchezo, ameulizwa na Zaka Zakazi sababu za kutocheza kwenye mchezo, na mwenyewe kueleza kuwa anasumbuliwa na majeraha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic