Kikosi cha Yanga kimerejea jijini Dar es Salaam tayari kuendelea na ratiba za maandalizi ya Ligi Kuu Bara.
Yanga ilikuwa Zanzibar kucheza mechi ya kirafiki iliyokuwa maalum kumuaga nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro'.
Kwa mujibu wa uongozi wa Yanga, mazoezi yataendelea kesho kwenye Uwanja wa Polisi, Kilwa Road jijini Dar es Salaam.
Tayari Yanga imecheza mechi sita na kukusanya pointi 16 katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.
0 COMMENTS:
Post a Comment