CHAMA ,OKWI,KICHUYA WALIPA KISASI KWA YANGA
Timu ya Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Stand United mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa leo ikiwa ni kulipa kisasi kwa wapinzani wao Yanga ambao nao walishinda kwa idadi ya mabao hayo jana.
Kiungo mchezeshaji Clatous Chama, mshambuliaji wa kimataifa Emanuel Okwi na kiungo mshambuliaji Shiza Kichuya wamewanyanyua mashabiki wa Simba .
Chama amefunga bao lake la kwanza dakika ya 31,amemtengenezea pasi ya bao Okwi dakika ya 45,Kichuya baada ya kupiga kona dk ya 77,mchezaji wa Stand United Eric Mulillo alijifunga na kuhitimisha ushindi mnono kwa Simba.
Kwa kweli ligi ni ngumu na kila inapopatikana nafasi Simba inabidi kushinda, ikumbukwe imeshaharibu mechi moja ya kule Mwanza. Kila la heri Simba kwenye mchezo wa leo.
ReplyDeleteProtas-Iringa
Hayo ndiyo maajabu sasa na stendi hawakufunga hata goli moja...timu iliyo namba 7 kuifunga iliyo namba 11.Siyo iliyo namba 3 ikiwafunga vibonde vya ligi mnatuandikia eti wamefanya maajabu...Saleh mnaboa timu yenu ikishinda vichwa vya habari mnavirembesha mnavipamba mpaka vinaboa.Timu zingine zikishinda ni habari ya kawaida.blog yenu inatia aibu
ReplyDeleteKichuya hajafunga goli lolote
ReplyDeleteHuo ndio umbumbu wa uandishi,like no own gaol LA erick murilo,unatuambiaje kichuya kafunga.Naona hukuwepo uwanjan hata azm hujaangalia tens unasfia,kona ya moja kwa moja,kuwa making kaka na uandishi wako,acha muisifie vyura fc but simba tupo juu zaid yao
ReplyDelete