DILUNGA AWAANGUKIA MASHABIKI SIMBA
Kiungo mshambuliaji wa Simba Hassan Dilunga amewataka mashabiki waendelee kuwapa sapoti hasa katika michezo yote ya ligi kuu bila kukata tamaa.
Dilunga ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa muda kutokana na kuwa majeruhi,leo atakuwa uwanjani wakati Simba wakicheza na Stand United, amesema kwa sasa yupo fiti kuonesha ushindani.
"Nipo vizuri kwa sasa namshukuru Mungu,kikubwa tu nawaomba mashabiki waendelee kutupa sapoti katika michezo ambayo tutacheza kwani ushindani ni mkubwa kwenye ligi"alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment