October 21, 2018




ALIYEKUWA straika wa zamani wa Yanga, Obrey Chirwa jana aliibukia Taifa na kuiangalia timu yake wakati ikiwa inapata ushindi huo wa mabao 3-0  dhidi ya Alliance Schools ya Mwanza.

Chirwa ambaye aliondoka mwanzoni mwa usajili wa msimu huu baada ya mkataba wake kumalizika alikuwa jukwaani eneo la V.I.P akiwaangalia Yanga jinsi ambavyo walikuwa wanacheza na kumshuhudia straika aliyechukua nafasi yake, Heritier Makambo akifunga moja ya bao yaliyoipa ushindi timu hiyo.
Chirwa kwa sasa anacheza ndani ya kikosi cha Nogotoom cha Misri ambapo mambo yake yamekuwa magumu baada ya kukumbwa na ukata wa kutupia mabao.

Mashabiki wa Yanga ambao walijitokeza uwanjani baada ya kumuona mshambuliaji huyo walianza kumpigia makofi na kuimba kwa kulitaja jina lake.

Habari ambazo Spoti Xtra, limezipata ni kwamba mshambuliaji huyo raia wa Zambia yupo nchini na anaweza kumalizana na moja ya timu kati ya Yanga au Azam FC katika dirisha dogo la usajili ambalo litafunguliwa Novemba 15, mwaka huu.

Spoti Xtra, lilimbana mwenyekiti wa usajili wa Yanga, Hussein Nyika aliyekuwa amekaa nae jukwaani kutaka kujua lolote kuhusika na ujio wa straika huyo ambapo alisema: “Subirini hadi usajili ufunguliwe ndiyo tutaeleza lakini siyo kwa sasa.” Lakini Chirwa alidai yuko likizo hivyo aliamua tu kuwatembelea Yanga ingawa Spoti Xtra linajua kuna kitu kinaendelea.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic