Mpiga picha na mwongozaji wa video za Wasafi, Lukamba amefanya mahojiano na Global TV Online baafda ya kuzawadiwa gari mpya aina ya Toyota, Alteeza na msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz.
Katika mahojiano hayo Lukamba amesema kuwa amekuwa akitumiwa meseji nyingi kupitia Insta Dm, huku wakimwagia sifa mbalimbali, Pia amefunguka kuwa gari aliyopewa na bosi wake akatwi chochote kwenye mshahara wake.
Alichokisema Diamond wakati anamzawadia Lukamba zawadi ya gari
“Lukamba anakaa Bunju, kuna kipindi alikabwa na kuchukuliwa hadi laptop sasa leo nampatia gari,” aliyasema Diamond Platnumz akiwa katika tafrija aliyoifanya mitaa ya Tandale Sokoni katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo aligawa misaada mbalimbali kwa wananchi wa Tandale.
0 COMMENTS:
Post a Comment