Kama iliyo ada washindi kupitia promosheni ya Shinda Zaidi na SportPesa wameendelea kukabidhiwa zawwadi zao za Bajaji mara baada ya kucheza na kuingia kwenye droo inayoendeshwa na kampuni ya michezo ya kubashiri, SportPesa.
Ilikuwa ni zamu ya kukabidhi Bajaj kwa Mecksedeck Mguba (26), Fundi Seremala, mkazi wa Mabibo jijini Dar es Salaam.
Mguba akieleza juu ya furaha yake baada ya kushinda, alisema kwa mara ya kwanza alipopata taarifa za ushindi wake hakuamini hadi pale alipokutana na timu ya SportPesa kuja kukabidhiwa Bajaj yake
Mguba pia akieleza juu ya malengo yake, alisema kwa sasa anatarajia kuweka akiba ya fedha atakazokusanya kupitia Bajaj hiyo ili kujenga nyumba yake kwakuw sa sasa anaishi kwenye nyumba ya walezi wake.
Naye baba mdogo ambaye ndiye mlezi wa Meck, alisema furaha yake imepitiliza na tukio hilo analichukulia kama baraka kwa familia yake.
Mecksedeck Mguba ni mshindi wa droo ya kumi ya shinda zaidi na SportPesa, na anajumuika na washindi wengine wa droo zilizopita kuanza maisha mapya ya kutafuta mafanikio.
Shinda zaidi na SportPesa ni promosheni maalumu kwa watu wote wanaobashiri na kampuni hiyo, ambapo kila anayebashiri anaingia moja kwa moja kwenye droo ya kujishindia Bajaj mpya kwa muda wa siku mia moja.
Wakati huo huo SportPesa wamerahisisha utaratibu wa kujisajili na kucheza, kwa watu wote wenye aina zote za simu, iwe simu za kufuta "smartphone" au simu za kawaida maarufu kama simu za "kitochi" kwa kubofya tu *150*87#
Kwa upande Mwingine Leo sportPesa wamepata mshindi wa 13 wa Shinda zaidi na sportPesa Bwana Hassan Fares kutoka Tunduru Ruvuma ambaye anaungana na washindi kumi na Mbili ambao mpaka sasa wameshinda bajaji zinazotolewa na SportPesa kila siku kwa yeyote anayetupia ubashiri wake.
Akizungumza na waandishi wa Habari Mara baada ya Droo ya 13 kuchezeshwa Mkurugenzi wa utawala na Udhibiti kutoka SporPesa, Tarimba Abbas Alisema mpaka hivi sasa Tayari Jiji la Dar es salaam limeshapata washindi wanne ambao wameshinda Bajaji na Nyingine zilizobaki zimetua mikoani.
Tarimba amewasisitiza Watanzania kucheza Mara nyingi wawezavyo kwani Bajaji Bado zipo za kutosha na kwa kila anayecheza ana Nafasi kubwa ya Kuibuka mshindi.
"Mpaka sasa hivi Dar es salaam ilishapata washindi wanne na bajaji nyingine zimeenda mikoani hivyo niwaombe watanzania kuchangamkia Fursa kwa sababu nafasi ya kushinda bado ipo kubwa kwa kila anayebashiri anaingia kwenye droo huu ndio wakati wa kuitumia fursa hii kutoka sportPesa," alisema Tarimba.
Kiongozi huyo amesema njia za kucheza na SportPesa ni Rahisi na inawezekana kwa kutumia simu yeyote ya mkononi ambapo mtu anaweza kucheza kwa Kubofya *150*87# au akacheza kwa kutumia tovuti yani www.sportpesa.co.tz, Njia nyingine ni kucheza kwa kupakua App ya sportPesa ambayo hii unaipakua moja kwa moja kutoka kwenye tovuti sportpesa.co.tz.
0 COMMENTS:
Post a Comment