Pamoja na wengi kumuangalia zaidi Jose Mourinho wa Manchester United, Kocha wa Madrid, Julen Lopetegui anaonekana ndiye kocha mwenye hofu zaidi ya kupoteza kibarua chake, miezi 3 tu baada ya kuanza kazi.
Tayari kapoteza mechi ya ligi, Ligi ya Mabingwa, Kombe la Super Cup na harufu ya kufutwa kazi, tayari inanunikia.
Wakati anatua Madrid, mwanzoni kabisa ya michuano ya Kombe la Dunia, Lopetegui alionekana kuwa na wakati mgumu baada ya kuondoka kwa Kocha Zinedine Zidane.
Hata kama kocha huyo aliondoka, lakini kocha huyo raia wa Hispania alijiunga na Madrid baada ya nyota wake, Cristiano Ronaldo naye kuwa ameondoka na kujiunga na Juventus ya Italia.
Hii imemfanya kocha huyo kuzidi kuwa na wakati mgumu na sasa analazimika kutengeneza kila kitu upya.
Lakini ubaya wa Madrid ni kutochelewesha kocha anayeyumba na hii inamfanya kuwa kocha mwenye hofu zaidi na kazi yake kwa kipindi hiki.
0 COMMENTS:
Post a Comment