HARMONIZE AOKOA JAHAZI NDANDA
Baada ya kushindwa kurudi Mtwara kutokana na ukata ulioikumba timu ya Ndanda na kusababisha kubaki mkoani Singida, uongozi wa Ndanda FC uliamua kumuomba msanii Harmonize aweze kuwasaidia fedha ili warejee Mtwara kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Mbeya City.
Katibu wa Ndanda FC, Selemani Kachele alisema waliamua kumuomba Harmonize awasaidie kiasi cha fedha ambapo amekubali kuwasaidia.
Ameeleza kuwa baada ya kuwasiliana na msanii huyo amewaeleza kuwa kwa kuwa hayupo nchini, amesema atawasiliana na meneja wake, Babu Tale ili aweze kuwasaidia kwa chochote ambacho kitapatikana.
“Tayari tumeshawasiliana na Harmonize lakini kama unavyojua kwa sasa hayupo nchini yupo Marekani hivyo ametuambia anawasiliana na Babu Tale kwa ajili ya kuangalia ni jinsi gani atatusaidia.”.
Aidha, wakati gazeti hili likiingia mitamboni, ilielezwa kuwa Harmonize ametimiza ahadi yake kwa kutoa kiasi cha Sh milioni 3.5 kuisaidia timu hiyo
0 COMMENTS:
Post a Comment