SKENDO YA KUBAKA INAMPASUA KICHWA RONALDO
Staa wa Juventus, Cristiano Ronaldo amedai kuwa kuna watu walifoji taarifa zake kuhusu skendo ya ubakaji inayomuandama kwa sasa.
Ronaldo ameweka wazi hayo kupitia mwanasheria wake, Peter Christiansen ambaye amedai kuwa kuna nyaraka ziliibiwa na kutumika vibaya kwenye skendo hiyo ili kuonyesha ni kweli mteja wake alibaka kitu ambacho siyo kweli.
Mwanasheria huyo amesema baada ya nyaraka kadhaa kuibiwa zilitengenezwa na kubadilishwa ili ionekane Ronaldo alihusika katika kumshawishi mwanamke aliyefungua kesi kuwa alilipwa ili akae kimya miaka kadhaa ya nyuma.
Ronaldo, 33, amekuwa akikana mara kadhaa kuhusika katika kumbaka Kathryn Mayorga wakati walipokutana kwenye ukumbi wa starehe maeneo ya Las Vegas nchini Marekani mwaka 2009 lakini skendo hiyo imeendelea kumuandama na kutishia biashara zake binafsi.
Nyota huyo anadai lengo la skendo hiyo ni kumharibia sifa na jina lake na hakuna ukweli wowote.
I l i d a i w a kuwa mwaka 2010, R o n a l d o a l i m p a mw amk e huyo pauni 287,000 ili akae kimya kuhusu skendo hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment