October 8, 2018


Washambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi na Mnyarwanda, Meddie Kagere juzi Jumamosi wamezua balaa ndani ya timu hiyo baada ya kumalizika kwa mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya African Lyon, na kujikuta wakivamiwa na mashabiki wakati wakienda kupanda basi baada ya mechi.

Mashabiki wa timu hiyo waliwashutumu wachezaji hao kwa kutokuwa makini kuzitumia ipasavyo nafasi za kufunga wanazozipata uwanjani jambo ambalo limesababisha timu hiyo kupata ushindi kiduchu katika baadhi ya mechi zake ilizocheza mpaka sasa.

Licha ya Okwi kufunga bao moja katika mchezo huo wa juzi dhidi ya Lyon, lakini mashabiki walionekana kutoridhishwa na kiwango chake, hasa kutokana na kukosa nafasi nyingi.

Wakati Okwi na Kagare wakienda kupanda basi la timu hiyo kwa ajili ya kurudi kambini, walizongwa na kundi la mashabiki wa timu hiyo ambao walikuwa wakiwatuhumu kuwa wao ndiyo wanaongoza kupoteza nafasi za kufunga ndani ya kikosi hicho ukilinganisha na wachezaji wengine.

Hata hivyo, Okwi aliwajibu mashabiki hao kwa kuwaambia kuwa amewasikia hivyo watahakikisha wanalifanyia kazi tatizo hilo.

“Msiwe na wasiwasi, tumewasikia hivyo tutalifanyia kazi tatizo hilo,” alisema Okwi akiwaambia mashabiki hao.

Ndani ya mechi mbili za ligi kuu ambazo Simba imecheza hivi karibuni dhidi ya Yanga pamoja na ile ya juzi dhidi ya African Lyon, ilifanikiwa kutengeneza jumla ya nafasi 24 za kufunga lakini ni nafasi mbili tu ambazo ilizitumia.

Katika mchezo dhidi ya Yanga ambao Simba ilitawala kwa kiwango kikubwa, ilitengeneza nafasi 14 lakini hakuna nafasi hata moja ambayo ilitumika ipasavyo, juzi dhidi ya Lyon ilitengeneza nafasi 10 za kufunga lakini ni mbili tu ambazo iliweza kuzitumia ipasavyo.

CHANZO: CHAMPIONI

2 COMMENTS:

  1. Mtafanya kampeni ya chuki na husuda lakini haiwezi kuizuia Simba kutwaa ubingwa.Anayevamiwa nä anayevamia wanaongea? Au kuvamia ni neno jipya ?Mwingine kaandika Simba Ina pointi 13!!!!Ya Dante hii blogu hata haikudiriki kuandika. Simba Ina kikosi kipana sio cha kuungaunga.Chuki hazitasaidia kitu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mwandishi hajakulazimisha kusoma blog yake,ukiona hutendewi haki compile your programmes and quit!

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic