Lipuli FC wamelalamika wakiamini ratiba ya Ligi Kuu Bara si rafiki kwao.
Kocha Mkuu wa Lipuli FC, Selemani Matola amesema watawakaribisha Mbao FC kesho lakini bado watakuwa na uchovu wa safari.
Mbao FC inanolewa na kocha Amri Said ambaye alikuwa pamoja na Matola kabla ya kuhamia katika kikosi hicho cha Mwanza.
"Ratiba si nzuri kwetu, si rafiki kwa kuwa tumefika hata hatujapumzika lakini tunalazimika kucheza mechi.
"Tena usisahau, kuwa mechi ilikuwa Alhamisi imerudishwa Jumatano. Tunalazimika kucheza na tutafanya hivyo na tunataka kufanya vizuri," alisema.
Inaonekana bado mambo hayajawa vizuri kwa Lipuli FC kwani baada ya mechi tisa iko katika nafasi ya 14 baada ya kukusanya pointi tisa tu.
0 COMMENTS:
Post a Comment