October 8, 2018


Baada ya kuoneshwa mlango wa kutoka nje rasmi, Kocha Msaidizi wa Simba, Mrundi, Masoud Djuma, amesema kuondoka ndani ya wekundu wa Msimbazi si mwisho wa kuendelea na maisha mengine.

Djuma ambaye alitua Simba mnamo mwezi Oktoba 2017, aliteka vichwa vya habari baada ya kuripotiwa kukosa maelewano mazuri na Makocha wakuu tofauti ndani ya timu hiyo.

Mrundi huyo ameeleza kuwa kuondoka Simba ni mwanzo wa yeye kuendelea na maisha mengine ya soka na akisema kuwa Simba si sehemu pekee atakayokaa milele.

Kocha huyo aliingia kwenye migogoro na Mfaransa, Pierre Lechantre ambaye aliondoka na kumpa mikoba Mbelgiji Patrick Aussems ambaye anaendelea kukinoa kikosi cha Simba mpaka sasa.

Migogoro na kutokuelewana baina ya Djuma na wakuu wake yaliendelea kushika kasi, ikiwemo kuelezwa kusababisha chuki binafsi baina ya wachezaji na mkuu wake, jambo ambalo Aussems hakulifurahia.


4 COMMENTS:

  1. Aache tu ubinafsi kwani siku zote kwenda kuanza ajira mpya ni changamoto kweli kweli. Kazi za ukocha mara chache sana kuona kocha akifuatwa na mafanikioa aliyotoka nayo katika ajira yake iliyopita. Lakini ni mara nyingi sana kuona kocha akifuatwa na mikosi na matatizo aliyotokanayo katika ajira yake iliyopita. Pale Simba Masoud Djuma alishakubalika kilichompasa kufanya ni kuuvaa uanafamilia wa Simba na kujua yakwamba wageni wanaokuja wataondoka na yeye watamuacha tu. Watu wa siku hizi au tuseme vijana wengi wanakosa elimu maarifa jinsi ya kuishi na kufanya kazi na watu wengine kwa mafanikio,kila mtu anataka kuishi peke yake kimawazo na vitendo bila kujali hisia za watu wengine.

    ReplyDelete
  2. Pupa zimemponza Masoud. Alikuwa anahubiri maji anakunywa mvinyo. Alipewa ahadi akashindwa kusubiri.

    ReplyDelete
  3. Hawa waandishi uchwara kazi kuangalia Simba inafanya nini?
    Yanga Ina kocha deiwaka lakini hakuna anayeandika!!Uliona wapi kocha nsaidizi wa timu ya Taifa anakuwa kocha wa klabu kwa wakati mmoja???
    Ingekuwa Simba zingeandikwa vitabu wacha makala.

    ReplyDelete
  4. Alikuwa kirusi....kwani lazima afundishe Simbs?atafute timu nyingine.Simba aliikuta na ameiacha.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic