SILAHA ZA KIVITA ZILIVYOKUTWA KWENYE GARI ALILOTEKWA MO DEWJI – VIDEO
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amezungumzia tukio la kupatikana kwa mfanyabishara maarufu nchini, Mohammed Dewji kutoka kwenye mikono ya watekaji na kusema wamekuta silaha za kivita kwenye gari alilokuwa ametekwa MO.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 20, 2018, Sirro amesema; “Tulipofika hapa Gymkana tukalikuta gari lililomteka Mohammed Dewji likiwa limetelekezwa, tukaona tulizuie mtu asiingie kwanza tufanye upekuzi, tumekuta silaha ya kivita AK 47 moja na bastola tatu.
“Fikiria Mohammed Dewji amekuja amekuja kutekwa kwa silaha nne, bastola zilikuwa na risasi 16, na hii AK 47 ilikuwa na risasi 19, ni silaha nzito ya kivita, inaweza kupiga risasi 19 mfululizo. Kwenye biashara hii lazima tuwaonyeshe kuwa hii ni Tanzania, lazima tuwapate, na tukiwapata watueleze walikuwa wanataka kufanya nuini.
“Watekaji wa Mo Dewji walitaka kuichoma hii gari kupoteza ushahidi, wakajikuta mwisho wa siku wana mashaka na hilo. Inasemekana walikuwa wakizungumza Kiingereza na Kiswahili cha hovyohovyo, siwezi kusema wametoka nchi gani mpaka pale tutakapowatia mbaroni,” amesema IGP Sirro.
Mo Dewji alitekwa alitekwa alhamisi iliyopita, Oktoba 11, 2018 katika gym ya Hotel ya Colosseum iliyopo Oysterbay jijini Dar es salaam na kupatikana usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Gymkana baada ya kutelekezwa na watekaji hao.
0 COMMENTS:
Post a Comment