MONALISA AANGUA KILIO UKUMBINI, SABABU NI HII
Msanii wa filamu Bongo, Yvone Cherry ‘Monalisa’ hivi karibuni aliangua kilio ukumbini alipokuwa akizungumzia jinsi mabinti wanaotamani kuingia kwenye tasnia ya filamu wanavyonyanyaswa kingono sehemu wanazokwenda kuomba kusaidiwa.
Monalisa aliangua kilio hicho ndani ya Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo alikuwa akizindua mpango wa kuwaendeleza mabinti wenye vipaji vya kuigiza uitwao Monalisa ACT.
Katika tukio hilo, mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo; Juliana Shonza ambapo kabla ya kutoa hotuba, Monalisa alipanda jukwaani na kuanza kuelezea kilimchomsukuma kuanzisha mpango huo.
Mona alisema kuwa anajua mabinti wengi wakienda kwa watu kuomba kusaidiwa ili waoneshe vipaji vyao, wengi huishia kudhalilishwa kingono ndipo wasaidiwe, jambo ambalo alililaani vikali.
“Ukweli mabinti wengi wana vipaji vya filamu lakini wanaishia kukata tamaa na vipaji vyao kupotea, hii ni kwa sababu wanapokwenda kuomba msaada wameishia kuombwa rushwa ya ngono, jambo ambalo siyo zuri kabisa,” alisema Mona huku machozi yakimlengalenga na hata aliposhuka na kwenda kuwakumbatia baadhi ya mabinti alijikuta akilia.
0 COMMENTS:
Post a Comment