NI DABI KALI MBEYA LEO
Ndani ya Jiji la Mbeya, leo kuna ‘Mbeya Derby’ ambapo timu za Mbeya City na Tanzania Prisons zitapambana kwenye Uwanja wa Sokoine mjini hapa.
Prisons ambao ni wenyeji wa mchezo huo, katika michezo mitano iliyopita ya derby hiyo, Prisons imeshinda miwili huku Mbeya City wakijitutumua na kuambulia sare mara tatu.
Kocha wa Mbeya City, Ramadhan Nsanzurwimo raia wa Burundi alisema kuwa pamoja na uwezo mzuri na rekodi bora za Prisons ni lazima leo wamalize uteja kutokana na maandalizi kabambe waliyofanya.
“Hatujapata matokeo mazuri kwa kipindi cha hivi karibuni, hii inaonyesha jinsi gani huwa wanajipanga vizuri kutukabili lakini na sisi hatutakuwa nyuma ni lazima tuhakikishe tunapata matokeo mazuri ambayo ni pointi tatu muhimu,” alisema kocha huyo.
Naye Kocha wa Prisons, Abdallah Mohamed alisema: “Tumejipanga kuendeleza rekodi yetu ya kuwachapa Mbeya City japokuwa hatupo kwenye kiwango kizuri tangu kuanza kwa msimu huu lakini tunataka kupata ushindi hiyo kesho (leo).
0 COMMENTS:
Post a Comment