October 6, 2018


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mnigeria Emmanuel Amunike ameweka wazi kuwa sasa umefika wakati wa Stars kwenda kucheza fainali za michuano ya Kombe la Afrika (Afcon) baada ya kukaa kwa muda mrefu wakizishuhudia timu kutoka mataifa mengine zikishiriki.

Stars ambayo kwa sasa ipo kambini ikijiandaa na mchezo wa tatu wa kuwania kufuzu Afcon mwaka 2019, inatarajiwa kucheza ugenini dhidi ya Cape Verde, Ijumaa ijayo.

Amunike ameliambia Cham­pioni Jumamosi kuwa, amekuwa akiwasisitiza wachezaji kuwa umefika wakati wa mataifa men­gine kuishuhudia Tanzania ikishiriki Afcon, hivyo sasa mataifa hayo yanatakiwa kuishuhudia Stars ikishiriki michuano hiyo.

“Nimekuwa nikiwaambia kila siku wachezaji wangu kuwa wanapaswa kutumia vipaji vyao kuwapa taba­samu Watanzania, na hicho ndicho kitu pekee mtu anachotakiwa kuki­fanya katika maisha yake Watanzania wanahitaji kuiona timu yao ikishiriki Afcon mwakani.

“Kucheza Afcon kutaleta sifa kwa nchi na kutapandisha hadhi ya wachezaji, wanapaswa kufahamu njia ya mafanikio ina changamoto nyingi inatakiwa moyo wa kizalendo na dhamira ya kutaka mafanikio,” alisema Amunike.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic