October 13, 2018


Timu ya taifa ya Uganda imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Lesotho katika mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2019.

Mabao ya kipute hicho yamewekwa kimiani na Emmanuel Okwi aliyeingia kambani mara mbili na moja likifungwa na Farouk Miya.

Matokeo hayo yanaifanya Uganda kuwa juu ya msimamo ikifisha alama 7 katika kundi L huku Lesotho ikisalia nafasi yake ya 3 na pointi 2.

Timu hizo zitarudiana tena Oktoba 16 2018 ambapo Uganda watapaswa kusafiri kuelekea Lesotho kwa ajili ya kibarua hicho.

5 COMMENTS:

  1. Hongera okwi kwa kuisaidia timu yako

    ReplyDelete
  2. Waganda wapo serious na business.Mfano Taifa stars ikichapwa 3-0 mtungi na wa cape Verde waganda waliwatungua wa cape Verde goli moja mtungi pale pale cape Verde. Wakati Taifa Stars ilitabika kupata Sare na Lesotho katika uwanja wake wa nyumbani Dar,waganda inawabamiza Lesotho goli 3-0 mtungi.Lakini cha kufarahisha zaidi ule uti wa mgongo wa timu ya Taifa ya Uganda unaundwa na wachezaji wawili muhimu wanaocheza soka Tanzania sio ulaya. Hiyo Simba tunayoidharau na kuiona wachezaji wake si lolote si chochote waganda kwao ni moja klabu hazina kwa wachezaji wao wa Taifa. Kabla ya yote hebu tuungalie wasifu wa kocha wa timu ya Taifa ya Uganda Mfaransa Sebastian Desabre kulinganisha na kocha wa timu ya Taifa ya tanzania Emanuel Amunike. Desabre kabla ya kutua Uganda alikuwa alikuwa kocha wa timu ya Ismailia ya Egypt au Misri lakini alishawahi kufanya kazi nchi mbali mbali ulaya na Africa. Amefundisha klabu kadhaa za Africa kama Asec Mimosa Ivory coast, Waydad Casablanca Morocco,Alishafanya kazi Tunisia,Alishafundisha club Lebolo ya Angola,Alishafanya kazi Cameroon, Algeria, Dubai nakadhalika na inakadiriwa kuwa waganda wanamlipa Dolla $25000 elfu kwa mwezi. Sasa kwa mtizamo wa haraka haraka utagundua kiasi gani waganda walivyo makini na uteuzi wa kocha wao wa timu ya taifa.Na hata ile Sare ya stars kule Uganda ni bahati na uwezo wakuja kutufanya hapa kwetu wanao hilo halina shaka. Kwanza wana kocha alie na uzoefu wa soka la Africa na fitina zake.Ameshafundisha miongoni mwa nchi fitina kwenye soka la Africa na naziangalia cape Verde na Uganda zikisonga mbele kwenye kundi la Taifa stars si kwamba hatuna wachezaji wa kutupeleka Afcon la hasha kama kuna kipindi tanzania ina vijana wa kazi kwenye timu ya taifa basi ni wakati huu lakini wanaowasimamia sio .

    ReplyDelete
  3. Utamuacha vip Erasto Nyoni... Ibrahm Ajib.. Kichuyaaa... Hao ndo wazoefu na mechi za kimataifaa bana.

    ReplyDelete
  4. Kwani Amunike amefundisha timu ngapi kabla ya kuja hapa?Luna mchambuzi mmoja wa azam anasema kuna faida ya kuwana kocha aluyechezea timu kubwa kama barca lakin akasahau kutuambua wasifu wake katk ufundishaj,kucheza na kufundisha timu kubwa kuna tofaut sana,naomba CV ya amunike as a coach not a player mwenye nayo

    ReplyDelete
  5. alipotoa droo na Uganda coach alisifiwa sana leo kafungwa anapondwa sanaaa!!!!
    kila mtu ana comment kama vile yeye ni coach !!! wa TZ tubadilike bado hatuna wachezaji wa level ya Uganda na hata Coach wa Uganda akija TZ mambo tabaki kua vile vile na huu ndio ukweli !! tusubiri miaka miwili ijayo nadhani tutakua na wachezaji wengi wazuri na wa kimataifa !!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic