ZLATAN IBRAHIMOVIC KUREJEA OLD TRAFFORD
Zlatan Ibrahimovic ana umri wa miaka 37 na wengi wanaamini anaelekea kustaafu lakini habari ni kuwa kuna uwezekano kibao kikageuka na mkongwe huyo akarejea Manchester United.
Straika huyo ambaye kwa sasa anacheza soka Marekani ametajwa kuhusishwa na kurejea Old Trafford kuungana na kocha wake wa zamani, Jose Mourinho ambaye yupo kwenye wakati mgumu kutokana na timu hiyo kutokuwa na matokeo mazuri.
Tetesi hizo zimeendelea kushika kasi kutokana na uhaba wa mabao ambao United imekuwa nao hasa kutokana na washambuliaji wake, Romelu Lukaku na Alexis Sanchez kutokuwa katika kiwango bora cha kufunga.
Watu wa karibu na Mourinho wameeleza kuwa mkongwe huyo anayeichezea LA Galaxy anaweza kurejea ikiwa atazungumza vizuri na Mourinho kumsaidia kumalizia msimu huu wa 2018/19.
Ikiwa itatokea hivyo haitakuwa mara ya kwanza kwa mchezaji anayecheza Ligi Kuu ya Marekani (MLS) kurejea Premier League kwa muda, iliwahi kutokea hivyo kwa Landon Donovan alipojiunga na Everton pia Thiery Henry alijiunga na Arsenal.
0 COMMENTS:
Post a Comment