Mabao pekee ya mchezo huo yamefungwa na Mrisho Ngassa pamoja na Emmanuel Martin.
Yanga imecheza mechi hiyo visiwani Zanzibar ikiwa ni sehemu ya kumuaga beki wake wa zamani, Nadri Haroub 'Cannavaro' ambaye amestaafu kucheza soka.
Cannavaro ambaye kwa sasa ni Meneja wa timu, ameagwa vema kutokana na timu yake kucheza soka zuri dhidi ya wapinzani kwa kutawala sehemu kubwa ya mchezo huo.
Mbali na kumuaga Cannavaro, Yanga imeutumia pia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi kuelekea mechi na Alliance Schools katika Ligi Kuu Bara.
0 COMMENTS:
Post a Comment