October 26, 2018


Beki Ally Ally wa KMC maarufu kama Ally Mwarabu, ndiye mchezaji aliyepiga mipira mingi ya vichwa katika mechi yao dhidi ya Yanga, jana.

Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa, KMC ililala kwa bao 1-0 lililofungwa na Fei Toto katika dakika ya 90 baada ya Ally kumuangusha Herietier Makambo wakati akiingia katika lango la KMC.

Mkwaju wa faulo wa Fei Toto, kiungo myumbulifu wa Yanga ndio uliozaa bao hilo la ushindi dakika za lala salama.

Lakini Ally Mwarabu ndiye aliyekuwa beki aliyepiga mipira zaidi ya 18 ya vichwa kati ya 20 aliyoruka na wachezaji wa Yanga.

Pamoja na kuwa na umbo dogo, Ally aliruka mara nne na Makambo ambaye ni mrefu na kufanikiwa kupiga mipira mitatu dhidi ya Mkongo huyo. 

Lakini mara nyingine, alionekana kufanikiwa kupiga mipira yote ya juu kwa asilimia 98.








2 COMMENTS:

  1. Nampenda Kocha Wa Yanga,Yeye kwake hafuati Mpira unaochezwa na magazeti,Imekuwa ni mila ya soka LA Tz.magazeti ndio yanampanga mcgezaji na kumwinua.lkn tubapo mwangalia nchezaji hiyo hana lolote..Ebu msikilize Zahera anacho sema juu ya Ajibu.yatazame magazeti yasemavyo.msikil8ze kocha mwingine Wa Taiga anavyozungumza juu ya Ajibu,.hao makocha wamfanana mtazamo.tuwaachie timu Tz inaenda kuwa nzuri so muda mrefu.lkn Zahera pia anacho kitu cha ziada.anauwezo Wa kusoma mchezo na kuleta mabadiliko ya uchezaji,wachezaju ili kuleta matokeo.Kwa hill kafaulu sana kocha hiyo

    ReplyDelete
  2. Alipania sana ndio maana akasababisha faulo za kijinga!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic