Kiungo kinda wa Yanga, Feisal Salim 'Fei Toto', sasa ndiye gumzo baada ya ule mkwaju wake wa adhabu ulioimaliza KMC dakika ya 90.
Fei Toto, amemfunga kipa mkongwe nchini, Juma Kaseja ambaye wakati anaanza kudaka mwaka 2000 katika timu ya Ligi Kuu Bara, Fei Toto alikuwa hajaanza hata darasa la kwanza.
Kwa sasa, Fei Toto ana umri wa miaka 20 akiwa njiani kutua 21, maana yake wakati Kaseja akiwa ligi kuu, yeye ndiyo alikuwa anaingia miaka minne kwenda mitano.
Kiungo huyo amekuwa gumzo kubwa kuanzia jana usiku baada ya Yanga kushinda kwa bao hilo 1-0 katika dakika za "lala kwa buriani".
Fei Toto alipiga faulo hiyo baada Herietier Makambo kuangushwa na Ally Ally wakati akienda kwenye lango la KMC.
Pamoja na Kaseja kuupanga ukuta wake kwa sekunde kadhaa akihakikisha umekaa sawa, Toto alipiga mkwaju huo kitaalamu zaidi na kuandika bao pekee la mchezo huo.
Acha uongo muandishi takwimu zako za uongo,mwaka 2000 huyo Dogo alikua na miaka 2.5.sasa wewe unatudanganya,alafu mpira hauna hivyo kijana,mbona kuna watu wana miaka 60 wanaoa wasichana Wa miaka 20 na wanaishi usiwe mjinga we we.
ReplyDeletePovu la nini!?? Jenga hoja, kutukana hakukupunguzii maumivu bali kunaonyesha uwezo wako mdogo wa kufikiri
DeleteMwandishi akiandika vitu kama vile hana akiri hata kiduchu ya kufikiria anapaswa kuandika...hamna MTU mzima anapenda kusoma pumba habari zisizo na mvuto. ..hii kipi cha ajabu mchezaji kijana akamfunga mchezaji mzee ambaye alianza kucheza soka LA kulipwa zamani..hata thamani ya Rinaldo na Messi hivi sasa imeshuka..Hii ni kwa sababu kiwango cha soka hushuka na umri..Inawezekana sana miaka mitatu iliyopita Kaseja angeurukia na kuupangua mkwaju wa Fei.Waandishi wengine wanaandika kishabiki.Yamkini huyu ndiye mwandishi aliyeandika kichwa cha habari Maajabu Yanga kuifunga Allience 3-0.Kiuhalisia Yale ni matokeo yaliyokuwa yanategemewa..Je si Simba alipopiga MTU mkono angeandika Basi maajabu makuu au ya dunia..Sio kutoa povu ila kama uaandika upuuzi haipendezi na kama haipendezi Basi watu watatoa povu..Mwandishi haujui critical thinking, logic yeyote na unatoa fikirio potofu..Acha kuandika kama vile wewe ni kihiyo wa darasa LA saba..jitahidi unaweza Fanya kazi bora zaidi..watu hupenda kazi bora na sio upuuzi...Basi use unaandika na jina lako kama wenzako wa binzuberi,IPP na Mwananchi.
DeleteKaseja aliua mzuka wa vijana kwa kuwafundisha ujinga wa kupoteza muda ili wapate suluhu, matokeo yake kawauza kwa bao la jioni. Dawa pekee ya kujilinda ni kushambulia.
ReplyDeleteWacha yanga tule mapointiiii
ReplyDelete